NEWS HOME MAGAZINE
Kila tarehe 7 July, ulimwengu mzima wa sherekeya Siku kuu ya lugha bora na tukufu la Kiswahili, moja wapo ya lugha zinazo tumiwa kwa uwingi ndani ya vyombo vya habari hapa mjini.
Wengi waandishi habari, waripoti habari zao katika lugha hiyo eneo nzima la maziwa makuu tulimo, huku habari ziki sikika katika inchi zote hizo za Kanda.
Katika miaka ya 1950, Umoja wa Mataifa ulianzisha “Kitengo cha Lugha ya Kiswahili” ndani ya Redio ya Umoja wa Mataifa, na kufanya Kiswahili kuwa lugha pekee ya Kiafrika iliyopo ndani ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Kimataifa ya Umoja wa Mataifa.
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, kupitia azimio lake 71/328, la tarehe 11 Septemba 2017 na kuhusiana na lugha nyingi, lilikaribisha utekelezaji wa siku maalum kwa kila lugha yake rasmi ili kufahamisha na kukuza ufahamu wa historia zao. Tamaduni zao na matumizi yao, lakini pia kuhimiza Katibu Mkuu na taasisi kama UNESCO kuzingatia kupanua mpango huu muhimu kwa lugha zingine zisizo rasmi zinazozungumzwa ulimwenguni.
*JOVIAL ELIEZER*
503900vue(s)